Bodi ya mkopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imetangaza kufunguliwa kwa dirisha la kukata rufaa kwa wanafunzi wote waliokosa mkopo au ambao hawajaridhika na kiwango cha mkopo walichopangiwa kwa mwaka wa masomo 2020/2021. Dirisha la kukata rufaa ya mkopo litakuwa wazi kuanzia tarehe 02/12/2020 mpaka 09/12/2020. Hivyo wanafunzi wote waliokosa mkopo au ambao hawajaridhika na viwango walivyopangiwa mnashauriwa kutumia fursa hii ya kukata rufaa. Picha ifuatayo inaonyesha hatua zote kwa ufupi Hatua muhimu za kufuata wakati wa kukata rufaa ya mkopo wa elimu ya juu 1. Tembelea tovuti ya bodi ya mkopo ya wanafunzi wa elimu ya juu. Tembelea tovuti ya bodi ya mkopo ili uweze kukata rufaa. Bofya Bodi ya mkopo (HESLB) ili uingie kwenye tovuti ya bodi ya mkopo, kisha bofya vitufe vitatu vinavyoonekana upande wa kushoto juu. Angalia picha ifuatayo kwa marejeo 2. Bofya kitufe kilichoandikwa appeal now Mara baada ya kubofya vitufe vitatu apo juu, angalia kitufe chenye rangi ya kijani kili...
Zoezi la usajili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha kilimo cha sokoine linaendelea na wanafunzi bado wanaendelea kusajiliwa. Muendelezo was zoezi la usajili Ukiachilia mbali changamoto ndogondogo zilizopo katik zoezi zima la usajili, uongozi wa chuo kikuu cha SUA umejipanga kutatua changamoto mbali mbali zinazowakumb wanafunzi kipindi hiki cha usajili. Aidha uongozi wa wanafunzi wa chuo kikuu cha kilimo cha sokoine SUASO kwa ushirikiano mzuri na viongozi wa dini mbalimbali zilizopo SUA, wamehakikisha wanafunzi wapya wa 2020/2021 wanahudumiwa vizuri na katika hali ya usalama. Pamoja na hayo uongozi wa jumuiya ya waislam katika chuo cha SUA (MSASUA) wakishirikiana na uongozi wa wanafunzi wa SUA (SUASO) wamehakikisha wanafunzi wapya wanafanikiwa kwa wepesi katika usajili wao. Japokuwa umakini wa wanafunzi wapya umekuwa mdogo, hususani kwenye nyaraka zao muhimu kama vyeti, simu na mabegi, MSASUA, SUASO na vikundi vingine wamejitahidi ku...