Zoezi la usajili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha kilimo cha sokoine linaendelea na wanafunzi bado wanaendelea kusajiliwa.
Muendelezo was zoezi la usajili |
Ukiachilia mbali changamoto ndogondogo zilizopo katik zoezi zima la usajili, uongozi wa chuo kikuu cha SUA umejipanga kutatua changamoto mbali mbali zinazowakumb wanafunzi kipindi hiki cha usajili.
Aidha uongozi wa wanafunzi wa chuo kikuu cha kilimo cha sokoine SUASO kwa ushirikiano mzuri na viongozi wa dini mbalimbali zilizopo SUA, wamehakikisha wanafunzi wapya wa 2020/2021 wanahudumiwa vizuri na katika hali ya usalama.
Pamoja na hayo uongozi wa jumuiya ya waislam katika chuo cha SUA (MSASUA) wakishirikiana na uongozi wa wanafunzi wa SUA (SUASO) wamehakikisha wanafunzi wapya wanafanikiwa kwa wepesi katika usajili wao.
Japokuwa umakini wa wanafunzi wapya umekuwa mdogo, hususani kwenye nyaraka zao muhimu kama vyeti, simu na mabegi, MSASUA, SUASO na vikundi vingine wamejitahidi kusaidia upatikanaji wa vitu vinavyopotoea.
Mwisho ashukuriwe Allah kwa kutupa uhai na afya mpaka tukafanikiwa katika zoezi Hili. Pia shukrani za dhati ziende kwa uongozi wa chuo, uongozi wa jumuiya mbalimbali za wanafunzi na watoa huduma wote kwa kurahisisha zoezi zima la usajili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza 2020/2021. Mpaka Sasa tunaelekea ukingoni mwa usajili wa wanafunzi, Allah awabariki Sana na awaongoze katika njia iliyonyooka.
Assalaam alykum,,,Karibuni sana SUA
ReplyDelete