Bodi ya mkopo ya wanafunzi wa elimu ya juu imetangaza kufunguliwa kwa dirisha la kukata rufaa kwa wanafunzi wote waliokosa mkopo au ambao hawajaridhika na kiwango cha mkopo walichopangiwa kwa mwaka wa masomo 2020/2021. Dirisha la kukata rufaa ya mkopo litakuwa wazi kuanzia tarehe 02/12/2020 mpaka 09/12/2020. Hivyo wanafunzi wote waliokosa mkopo au ambao hawajaridhika na viwango walivyopangiwa mnashauriwa kutumia fursa hii ya kukata rufaa. Picha ifuatayo inaonyesha hatua zote kwa ufupi
Hatua muhimu za kufuata wakati wa kukata rufaa ya mkopo wa elimu ya juu
1. Tembelea tovuti ya bodi ya mkopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.
Tembelea tovuti ya bodi ya mkopo ili uweze kukata rufaa. Bofya Bodi ya mkopo (HESLB) ili uingie kwenye tovuti ya bodi ya mkopo, kisha bofya vitufe vitatu vinavyoonekana upande wa kushoto juu. Angalia picha ifuatayo kwa marejeo
2. Bofya kitufe kilichoandikwa appeal now
Mara baada ya kubofya vitufe vitatu apo juu, angalia kitufe chenye rangi ya kijani kilichoandikwa Appeal now kisha bofya kitufe hicho ili uweze kujisajiri. Kwa marejeo tazama picha hii apa chini
Bofya appeal now |
3. Ingiza namba yako mtihani wa kidato cha nne (mfano: S0116.0011.2010)
Mara baada ya kubofya kitufe kilichoandikwa appeal now, ingiza namba yako ya kidato cha nne kwenye kisanduku kama utavyoona kwenye picha ifuatayo:
Ingiza namba ya kidato cha nne |
4. Bofya kitufe kilichoandikwa sign in
Baada ya kukamilisha usajili katika mfumo wa kukata rufaa, bofya kitufe kilichoandikwa sign in ili uweze kuingia katika mfumo wa kukata rufaa. Kwa marejeo angalia picha hapa chini
Bofya sign in |
5. Ingiza namba yako ya kidato cha nne na nywila(password) yako kisha sign in (log in)
Baada ya kubofya kitufe cha sign in, ingiza username yako (namba yako ya kidato cha nne) na nywila (password) yako kisha bofya kitufe kilichoandikwa sign in kuingia katika mtandao. Angalia picha apa chini
Ingiza username na password |
6. Bofya vitufe vitatu upande wa kushoto juu
Mara baada ya kuingia kwenye mfumo wa kukata rufaa, bofya vitufe vitatu vinavyoonekana upande wa kushoto juu ili uweze kujaza taarifa zako za msingi. Tazama picha hapa chini kwa marejeo zaid
Bofya vitufe hapo juu |
7. Kamilisha taarifa zako kwa kubofya vitufe vyenye alama x nyekundu kisha jaza taarifa zako
Hakikisha unaweka taarifa sahihi kwenye kila kitufe chenye alama x nyekundu ili uweze kukamilisha rufaa yako. Tazama picha hapo chini
8. Viambatanisho au nyaraka muhimu
Ni muhimu kuwa na nyaraka zifuatazo;
1. Certified birth certificate (Cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa)
2. Nyaraka ya kutilia nguvu ombi lako (Supporting documents). Mfano wa nyaraka za kutilia nguvu ombi lako ni kama vile cheti cha kifo cha mzazi, Barua ya mfadhili kama ulifadhiliwa shule ulizosoma, Hati ya hosipitali kama upo kwenye kundi la watu wenye mahitaji maalum kama vile mlemavu n.k, Barua kutoka serikali ya mtaa, kijiji au kata inayothibitisha maisha yako n.k
Ahsanteni saana kwa maelekezo mazuri, Allah awalipe
ReplyDeleteAllahumma ameen, atulipe sote
DeleteWe are proud to have you currently msasua leaders.
DeleteThanks ❤️
ReplyDelete